Mafunzo ya Vijana na Demokrasia : Jokate ataka vyama viwezeshe vijana wengi wagombee uongozi

Dar es Salaam, 06 Septemba 2024   ,Vijana washiriki mafunzo ya demokrasia na uwajibikaji chini ya mradi wa kuboresha uwajibikaji kwenye masuala ya demokrasia kwa wanawake na vijana ili kuboresha ujuzi wao katika utawala bora na uongozi wa kidemokrasia na uwajibikaji wa kisiasa katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania , mafunzo haya yameratibiwa na taasisi ya Imara Leadership Initiative Tanzania chini ya msaada wa Taasisi ya Kofi Annan Foundation , Ushirikiano wa Ulaya kwa Demokrasia (EPD), Taasisi ya Westminster ya Demokrasia (WFD), Kituo cha Oslo katika mradi unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya.

Tukio hilo, lililofanyika Dar es Salaam, lilihudhuriwa na Jokate Urban Mwegelo ambaye ni mwanachama wa WYDE Civic Engagement Network of Decision Makers na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tanzania pamoja na viongozi wengine wa vijana kutoka kwa makundi ya kisiasa, asasi za kiraia, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wanahabari.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Jokate Urban Mwegelo amewataka vijana kufanya mapinduzi kwa kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani. 

Jokate alisema hayo Dar es Salaam akifungua mafunzo ya vijana na demokrasia yaliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali Imara Leadership Initiative, ‘‘ Uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka huu na ule uchaguzi mkuu wa mwakani utakwenda kuamuliwa na vijana,sasa tusiwe tu sehemu ya kuchaguliwa kwa hiyo tujitokeze kwenye kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia ngazi za chini kwenye serikali za mitaa mpaka a juu bungeni’’ alisema.

Alisema uchaguzi uliopita idadi ya vijana ilikuwa ndogo hivyo uchaguzi wa mwaka huu wajitokeze kuchagua na kuchaguliwa pia ili wawe na jukumu la kupeleka maendeleo kwenye maeneo wanayoishi.

‘‘Na mgombee kuanzia ngazi za chini si juu tu maana kila kijana anataka kugombea ubinge, lakini niwaambie hayo mabunge hata kwenye ngazi za mitaani huko mnakoishi yapo, mnajadili matumizi ya fedha inayotolewa na serikali nyie mnfahamu hilo ? Nendeni mkagombee kuanzia huko alisema vyama vya siasa viwajengee vijana uwezo kwenye uongozi kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi asilimia kubwa ya watanzania ni vijana’’.

Mafunzo haya ni muhimu kwa vijana na wanawake kwa kuwa nchi inaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ambao utaanza mwishoni mwa Novemba 2024 huku ikitazamia uchaguzi mkuu mnamo 2025.

“Kwa kuwaunganisha vijana katika mafunzo yetu ya uwajibikaji ya WYDE, vijana katika demokrasia na wanawake wanapata fursa ya kujifunza demokrasia, lakini pia tunakuza kizazi cha viongozi ambao watahakikisha kukuza juhudi za uwajibikaji nchini”, alisema Petrider Paul, mwanachama wa Uwajibikaji wa WYDE nchini Tanzania.

‘Masuala ya uwajibikaji yanapaswa kuwa jukumu la kila mmoja ili kuhakikisha jamii yenye ustawi na maendeleo, vijana wameonyesha uongozi mahiri katika kuwezesha hamasa za masuala ya uwajibikaji nchini na pia vijana hawapaswi kuachana na michakato ya kisiasa haswa kuwania nafasi mbali mbali za uongozi nchini  ili kusaidia kuleta mabadiliko chanya ’ alisema Petro Ndolezi, Waziri Kivuli Ofisi ta Waziri Mkuu – Bunge , Sera, Vijana , Kazi na Ajira – ACT Wazalendo.

Mradi wa WYDE Accountability Hubs una lengo la kuwahamasisha wanawake na vijana kutoka Tanzania kuongeza ujuzi katika kukuza demokrasia na kufanya kazi pamoja na wanawake na vijana katika nafasi za uongozi zilizopo ambao wamekuwa muhimu katika kukuza demokrasia nchini.

MWISHO

Kuhusu Imara Leadership Initiative 

Imara Leadership Initiative ni taasisi isiyo ya kiserikali inayotekeleza miradi mbalimbali nchini ikiwemo ya utawala bora , afya , haki sawa kwa wanawake, mabadiliko ya tabia nchi katika kuwezesha maendelo nchini.

Kwa mawasiliano zaidi , tafadhali wasiliana nasi kupitia: 
Sarah Ernest
Afisa wa miradi  – ILI Tanzania 
Barua pepe : coordinator@imaraleadershipinitiative.org

Share your love