Kuhusu Mafunzo
Katika dunia ya leo inayozidi kuunganishwa na teknolojia, taarifa, na ushirikiano wa kimataifa, vijana wamepewa nafasi ya kipekee ya kushiriki katika majukwaa mbalimbali yanayoamua mustakabali wa jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Hata hivyo, fursa hizi mara nyingi hazijulikani vya kutosha, au vijana wengi wa Kitanzania wanapata changamoto za mbinu sahihi za kuzifikia na kuzitumia kwa manufaa yao na ya taifa.
Kupitia mafunzo haya, washiriki watajifunza
- Aina mbalimbali za fursa za kimataifa zinazopatikana kwa vijana
- Vigezo muhimu vinavyotakiwa ili kushiriki kwenye majukwaa hayo
- Njia za kuandika maombi bora na kuwasiliana kitaaluma na taasisi za kimataifa
- Ujuzi wa kujiamini, kuwasilisha hoja, na kuwakilisha taifa kwa heshima na weledi.
Makundi yatakayonufaika na mafunzo haya:
- Vijana wanaovutiwa na masuala ya uongozi, diplomasia, haki za binadamu, mazingira, au maendeleo ya jamii.
- Vijana wanaoshiriki kwenye shughuli za maendeleo katika ngazi za jamii, mashirika ya vijana au kamati za maendeleo.
- Wajumbe wa Mashirika ya Kijamii (CBOs) , Asasi za Kiraia (NGOs) na Asasi za Kimataifa (INGOs).
Wakati ni sasa vijana kuondoka kwenye muktadha wa kukaa kitaa na kuwakilisha Tanzania duniani.
Njia ya Uwasilishaji
Malipo : 30,000/=Tsh
Ufanisi Wako Sasa Upo Katika Mfumo wa Kidijitali!
Baada ya kukamilisha darasa hili kwa mafanikio, utapokea barua pepe kutoka kwa timu ya yetu ya Imara Leadership Initiative ikiwa na cheti chako